IGP SIRRO APANGUA MAKAMANDA WA POLISI
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Simon Sirro amemhamisha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Revocatus Malimi kutoka Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera kwenda makao makuu ya Polisi Dodoma na nafasi yake inachukuliwa na aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Awadhi Juma Haji.
IGP Sirro pia amemhamisha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Omary Said Nassiri kutoka Makao Makuu ya Polisi Zanzibar kwenda kuwa Kamnda wa Polisi mkoa wa Mjini Magharibi.
No comments