UVCCM Waungana kutoa Msaada wa Vifaa Hospitali ya Mwananyamala
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Comred Shaka Hamdu Shaka Leo ameungana na vijana wa Umoja wa Vijana wa Tawi La Mabibo Hostel katika Hospitali ya Mwananyamala ili kukabidhi vifaa vya hospital katika hospital hiyo.
Akipokea vifaa hivyo patron wa Hospitali hiyo Mussa Wambura amewashukuru sana, na amesema
“Tunashukuru kwa msaada huu utaokoa matatizo ya watoto, tunaomba muendelee na Moyo huu huu umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi hakika nyie ni vijana Wazalendo na wa mfano wa kuigwa” amesema mwakilishi wa Mganga Mkuu
Pia kwa upande wa Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Shaka hamdu Shaka amewashukuru wafanyakazi wa hospitali ya Mwananyamala ambapo amesema” Katika kuunga Mkono kwa vitendo kazi ya Mh Rais Magufuli leo tunakabidhi Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala vifaa hivi ambavyo ni mashine ya kuwasaidia akina mama wajawazito wakati wa kujifungua, Vaccum Extractor, BP Machine Clinical pamoja na Thermometer 15 na Tutaendelea kuguswa na Changamoto zingine katika utatuzi wa vifaa ”
na kuendelea kuwasisitiza watanzania wengine kuiga mfano “Hivyo tunawaomba wadau wa maendeleo na wote wanaoguswa na maendeleo wauunge mkono kauli mbiu yetu UVCCM Tukutane Kazini, tuendelee kushirikiana, UVCCM imeonyesha njia tunaomba wengine wafuate katika kuboresha Sekta ya Afya, elimu na uchumi kupitia makundi yote “
na kuendelea kuwasisitiza watanzania wengine kuiga mfano “Hivyo tunawaomba wadau wa maendeleo na wote wanaoguswa na maendeleo wauunge mkono kauli mbiu yetu UVCCM Tukutane Kazini, tuendelee kushirikiana, UVCCM imeonyesha njia tunaomba wengine wafuate katika kuboresha Sekta ya Afya, elimu na uchumi kupitia makundi yote “

Pia Amesisitiza kwamba Umoja wa Vijana unaendelea kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli katika kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi “Kitendo cha leo kukabidhi vifaa ni sehemu ya kukamilisha maendeleo endelevu Tutaendelea kumuunga mkono Rais wetu Magufuli kwa vitendo sio kwa maneno katika kufanikisha utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi 2015-2020”
Kaimu katibu Mkuu aliambatana na Katibu ya idara ya chipukizi na uhamasishaji wa Umoja wa Vijana UVCCM Jokate Mwegelo na maofisa wengine kutoka makao makuu ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi

No comments