TANGAZA NASISI

Breaking News

Album hii 'Kuibeba Imani' Itakubadilisha Maisha, Staa wa Gospel Joseph Mfangavo anakualika kuipokea Album yake hiyo


Mwimbaji wa nyimbo za injili anayekuja kwa kasi nchini Tanzania Bwana Joseph Mfangavo,anatarajia kutoa na album yake itwayo kuibeba Imani,ikiwa na lengo lakuimarisha jamii katika misingi ya kiroho.

Akizungumza na Gaditv.com mapema leo Bwana Mfangavo amesema jamii kubwa yakitanzania inahitaji kuimarishwa kiroho katika kuamini kiimani ili zisaidike kuondokokana na mitazamo hasi ambayo wengi wamekuwa wakiwa nayo kutokana nakupungukiwa na nguvu ya imani.

“wengi wamekuwa wakikosa Imani yakuendelea kutokana na shetani kuingia katikati mwa shughuli zao,hivyo mimi nimeamua kuleta Album inayokwenda kwa jina la Kuibeba Imani ili  iweze kuwafunza watanzania jinsi yakuwa na Imani pindi wawapo mahali popote pale bila kujali pito”

Hata hivyo Mfangavo amesema Album hiyo inayokwenda kwa jina la Kuibeba Imani niya pili na ina nyimbo kumi(10) huku yakwanza ikienda kwa jina la Fanya kazi ambayo ina jumla ya nyimbo nane(8),hivyo amewaomba Watanzania kwa ujumla kuipokea kazi yake mpya ili kila mmoja aweze kujifunza Kuibeba imani.

No comments