TANGAZA NASISI

Breaking News

Marekani Yaendelea kukomaa na IS


Waziri wa ulinzi wa Marekani Jim Mattis ameisihi Uturuki, mshirika wa jumuiya ya kujihami ya NATO, ilenge mashambulio yake dhidi ya wanamgabo wa dola la kiislamu tu nchini Syria. Kwa mujibu wa wizara ya ulinzi ya Marekani - Pentagon, waziri Mattis ametoa wito huo alipozungumza na waziri mwenzake wa Uturuki Nurettin Canikli, pembezoni mwa mkutano wa jumuiya ya NATO mjini Brussels.

Marekani inawaunga mkono wanamgambo wa kikurdi wa YPG kaskazini mwa Syria, wanamgambo wanaosaidia pakubwa pia katika juhudi za kupambana na wafuasi wa itikadi kali wa Dola la Kiislamu Daesh au IS. Uturuki inataka kuepusha kupata nguvu wanamgambo hao wa kikurdi ili kuzuia yasipate nguvu makundi ya wakurdi wanaopigania utawala wa ndani nchini Uturuki. Zaidi ya hayo serikali ya mjini Ankara imetangaza kuanzisha hujuma dhidi ya wanamgambo wa YPG katika mji wa Manbidj na kuwaonya wanajeshi wa Marekani waliowekwa sehemu hiyo, wasiingilie kati

No comments