MCH. PETER MSIGWA APELEKWA KAMATI YA MAADILI
Dk Tulia Ackson Mwansasu amempelekaMbunge wa Iringa Mch Peter Msigwakwenye Kamati ya Haki, Maadili naMadaraka ya Bunge ili akatoe ushahidiwake wa namna ufisadi ulivyofanyikakwenye mradi wa mfumo wa uhamiajimtandao (E-Immigration).
Tulia Ackson amesema hayo baada ya Msigwa kudai kuwa ana taarifa za kutoshajuu ya ufisadi uliofanyika katika mradiuliozinduliwa na Rais Magufuli hivikaribuni na kudai kuwa Kambi ya Upinzani bungeni wanazo nyaraka za kutosha ambazo hazina mashaka kuhusunamna ufisadi ulivyofanyika katika mradihuo chini ya Serikali ambayoinajipambanua kupambana na ufisadi. Kufuatia kauli hiyo ndipo hapo NaibuSpika aliagiza Mbunge huyo kwenda kutoa taarifa hizo kwa Kamati ya maadili.
"Mhe. Msigwa taarifa ulizonazo kuhusu ufisadi uliofanyika kwenye hili zoezi zipelekwe kwenye hii kamati, Kamati itakuja kulishauri bunge tufanye nini na huo ufisadi unaoendelea hayo maeneo kwa hiyo naiagiza kamati imuite Mhe. Peter Msigwa na yeye namuagiza Mhe. Msigwa apeleke huko hizo nyaraka ili bunge liweze kushauriwa na kuchukua hatua mahususi" alisema Tulia Ackson.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli Januari 31, 2018 alizindua Pasipoti Mpya ya Tanzania ya kielektroniki jijini Dar es Salaam.

No comments