TANGAZA NASISI

Breaking News

Mwanamuziki Wa Lithunia Aliekamatwa na kuhukumiwa kifungo cha maisha Jela kwa usafirishaji wa Dawa za Kulevya Tanzania

Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Moshi, imemhukumu kifungo cha maisha jela, Christina Biskasevskaja (26) raia wa nchi ya Lithuania baada ya kupatikana na hatia ya kusafirisha Dawa za Kulevya aina ya Heroin na Hydrochloride kinyume cha sheria .

Hukumu hiyo imetolewa Jana Mahakama kuu ya Tanzania, Kanda ya Moshi na Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu Aishieri Sumari ambapo upande wa utetezi ulikuwa ukiwakilishwa na Mawakili Patrick Paul na Gwakisa Sambohuku upande wa Jamhuri ukiwakilishwa na Jopo la Wanasheria wa serikali wakiongozwa na Tamari Mndeme .

Akisoma Hukumu, Jaji Sumari alieleza kuwa Mahakama imejiridhisha kupitia ushahidi usio na shaka uliowasilishwa na mashahidi wapatao saba wa upande wa Jamhuri unamtia hatiani mshtakiwa huyo ambao ulieleza kukutwa na Dawa hizo zikiwa na uzito wa Gramu 3775.26 na thamani yake Shilingi Milioni 169,886,700 za Kitanzania.

Biskasevskaja ambaye pia anatajwa kuwa msanii wa Muziki alikamatwa Augusti, 28 mwaka 2012 majira ya saa 9:16 za mchana katika uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA) wakati akijiandaa kuelekea katika mji wa Brussels Ubeligiji kupitia Addis Ababa Ethiopia.

1 comment: