TANGAZA NASISI

Breaking News

Nini Tafsiri ya Rais Zuma kugoma Kujiuzulu?


Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amesema kwamba hajafanya kosa lolotehivyo hawezi kujiuzulu kama chamachake cha African National Congress (ANCkilivyokuwa kikimtaka afanye leo.
Rais Zuma ameyasema hayo alipokuwaakifanya mahojiano na kituo cha runingacha SABC cha Afrika Kusinibaada ya chama chake kumtaka kujiuzulu kabla ya siku kuisha ama vinginevyo bunge litapigakura ya kutokuwa na imani naye kesho.
Kumekuwepo na mashinikizo mbalimbaliya kumtaka Rais Zuma ajiuzulu kutokanana tuhuma mbalimbali za rushwazinazomkabili.
Rais Zuma amesemachama hicho nawengine wote wanaomtaka ajiuzuluhawamtendei haki kwa sababu hakuna  hata mmoja anayetoa sababu au kumwambia ametenda kosa gani hadikustahili kujiuzulu.
Zuma amesema kwamba hapingani nachama hicholakini hakubaliani nauamuzi wanaotaka kuuchukua wakumshinikiza ajiuzuluAmesema alikubalikujiuzulu baada ya mwezi Junilakiniwalimkatalia.
Amesema kwamba licha ya mahojianoaliyoyafanya atatoa taarifa zaidi kuhusushinikizo hiloAidhaANC wamesemakwamba wamesikia kauli ya Rais Zuma nakwamba watatoa taarifa kamili baada ya kupata taarifa rasmi ya kiongozi huyo.
Mapemakiongozi wa ANC, Jackson Mthembu alisema kuwa, kura ya kutokuwa na imani na Rais itapigwabungeni Alhamisi ili Rais aondolewe, na Mwenyekiti wa ANC, Cyril Ramaphosa aatapishwa mara moja kuliongoza taifa hilo.
Kamati Kuu ya ANC ilikubaliana siku ya Jumanne kwamba Rais Zuma ajiuzulu ambapo walimtaka kufanya hivyo kabla ya Jumatano kuisha.
Wakati wa mahojiano yake, Rais Zuma hakuzungumzia jambo lolote kuhusu familia ya Guptas, ambayo inadaiwa kutumia ukaribu wake na Rais Zuma, kufanya ushawishi katika masuala mbalimbali ya kisiasa na kiuchumi nchini Afrika Kusini.

No comments