Ofisi ya Mkuu wa mkoa Arusha Kuchunguza Sekta Binafsi
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha imesema kuanzia Jumatano ya Februari 15, 2018 itatuma timu maalum ya uchunguzi, kwa wamiliki wote wa kampuni, mashirika na taasisi za Sekta binafsi zilizomo mkoani humo.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na ofisi hiyo, ilieleza kwamba timu hiyo ita angalia, kuhakiki pamoja na kutathimini jinsi sheria za kazi zinavyotekelezwa na vyombo hivyo.
Ilieleza kuwa, lengo la kuundwa timu hiyo ni kutoa elimu sambamba na kuangalia usalama mahala pa kazi ili kuhakikisha mazingira bora, wezeshi na endelevu yanakuwepo kwenye sekta binafsi katika utekelezaji wa majumu ya kazi kati ya waajiriwa na waajiri, pmaoja na kuhakikisha haki na stahiki za wafanyakazi wake zinalindwa na kuzingatiwa ipasavyo.
Taarifa hiyo iliongeza kuwa, kutokana na utaratibu wa usikilizwaji kero mbalimbali za wananchi wa mkoa wa Arusha unaofanywa na dawati la mkoa na Mkuu wa Mkoa huo, imebainika kwamba kuna migogoro mingi kazi kulingana na malalamiko yaliyotolewa na baadhi ya wananchi waliofika kwenye dawati hilo.
No comments