Uturuki imeagiza kuachiwa huru Mwandishi wa Habari aliyekaa zaidi ya mwaka Kizuizini, Wanasheria wataka afungwe jela Miaka 18
Uturuki imeagiza kuachiwa huru kwa mwandishi wa habari wa Ujerumani mwenye asili ya Uturuki Deniz Yucel anayeshikiliwa kwa zaidi ya mwaka mmoja bila ya kusomewa mashitaka, hatua itakayoondoa kihunzi kikubwa katika kuboresha mahusiano kati ya Uturuki na Ujerumani. Gazeti la Ujerumani ambalo ni mwajiri wa mwandishi huyo la Die Welt liliandika "Deniz Yucel yuko huru". Shirika la habari linalomilikiwa na serikali nchini Uturuki, limethibitisha kuachiwa huru kwa dhamana kwa mwandishi huyo kutoka kuzuizi cha kabla ya kusomewa mashitaka.
Alikuwa anatuhumiwa kwa makosa ya uhalifu wa kueneza propaganda na uchochezi. Wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani imethibitisha kwamba Yucel aliachiwa huru, na kusema kuwa imefurahishwa na hatua hiyo. Taarifa hiyo iliwafurahisha wafuasi wengi wa Yucel, ingawa bado wingu bado limegubika kesi hiyo, baada ya vyombo vya habari vya Uturuki kuripoti kwamba wanasheria wameomba Yucel aadhibiwe kifungo cha miaka 18 jela. Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani, Sigmar Gabriel amesema kuwa amri ya mahakama ya kumuachia huru haikuwa na masharti yoyote.

No comments