TANGAZA NASISI

Breaking News

DIWANI KINABO AUNGANA NA WAISLAMU MAONESHO YA WATOTO WALIOHITMU MAFUNDISHO YA QURAN TAKATIFU






Diwani wa Kata ya Themi Jijini Arusha Mh. Melance Kinabo ameungana na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Maonesho ya Mahafali ya watoto walifuzu mafunzo ya Quran TakatifuTakatifu hafla iliyofanyika katika msikiti wa Masjid Anwar Lemara Kati.


 katika Hafla hiyo watoto hao walipewa fursa ya kuonesha yale ambayo wamejifunza katika Madrasa ikiwa ni pamoja na mafundisho ya Imani ya dini hiyo na Kitabu Takatifu cha Quran.

Watoto walionesha uwezo mkubwa wa kukidadafua Kitabu hicho kwa kutoa mawaidha kwa Wazazi wao na halaiki huku wakitumia lugha ya Kiswahili na lugha ya Kimombo (Kingereza)



Katika Hotuba Yake Diwani Kinabo akawaomba Waasisi na Viongozi waandamizi wa dini hiyo kuendelea kujenga Taifa imara la kesho kwa kuwekeza kwa watoto kupewa elimu ya imani ya dini na mafunzo mema ya dini ili kuepukana na Taifa la vijana hovyo.

Kinabo amesema ni muhimu taasisi za Kidini kuungana kujenga Taifa imara kwa kuwalea watoto katika misingi ya Imani Takatifu.


 Aidha Masomo mengine yaliyojiri katika Maonesho hayo kwa upande wa wazazi wametakiwa Kuhakikisha wanafuatilia mienendo ya watoto wao katika maisha yao ya kila siku.


Hata hivyo Diwani  Kinabo akawatakia wananchi wote wa jiji la Arusha mfungo mwema wa mwezi mtukufu wa ramadhani.

HABARI MPYA HIVI PUNDE 

No comments