JKT Waendeleza Ubabe Kombe la Meya Dar
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam, Issaya Mwita akizungumza jambo katika hafla hiyo.
Mashabiki kutoka makao makuu ya JKT wakishangilia ushindi baada ya kukabidhiwa kombe lao.
JESHI la Kujenga Taifa (JKT) wameendeleza ubabe baada ya kufanikiwa kutetea ubingwa wao katika mashindano ya Kombe la Mstahiki Meya kwa mchezo wa Ngumi.
Michuano hiyo ambayo inasimamiwa na Mstahiki Meya wa Dar es Salaam, Isaya Mwita ilimalizika jana katika Uwanja wa Taifa wa Ndani na mshindi kuweza kukabidhi zawadi.
JKT walinafakiwa kutwaa ubingwa huo baada ya kupata pointi 10 katika mchezo huo huku mshindi wa pili akiwa ni Mzizima(Timu ya Mkoa wa Dar es Salaam) ambao walipata pointi nane na mshindi wa tatu akiwa ni Halmashauri ya Ubungo.
No comments