TANGAZA NASISI

Breaking News

JOHNSON MAHUMA Aula kwenye Jukwaa la Wafanyabiashara aliloongoza Waziri Mwakyembe Arusha


Aliyewahi kuwa Mgombea Udiwani kata ya Muriet kwa Ticketi ya Chama cha ACT-Wazalendo Mh. Johnson Mahuma Amesifu jitihada za Serikali kuwa kutanisha na kuwaelimisha wafanyabiashara wadogo wadogo.

Akizungumza katika hafla iliyo andaliwa na taasisi ya Magazeti ya Serikali TSN Bw. Johnson amesema majukwaa kama hayo yanewezesha kufahamu sehemu ambapo  Serikali inapata ugumu wowote kuwafikia wafanyabiashara lakini pia changamoto zinazoilabili sekta ya biashara nchini.

Aidha  Bw. Mahuma amesema licha ya jitihada mbali mbali zinazoendelea bado Wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama Machinga wanakumbwa na adha ya uhaba wa maeneo ya kufanyia biashara hivyo kuitaka Serikali kuandaa maeneo tengefu Kwa ajili ya Wafanyabiashara wadogo.

No comments