TANGAZA NASISI

Breaking News

MBOWE: KIFO NI UPATANISHO SOTE TUTARUDI TULIKOTOKA...

WABUNGE waBunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mei 29, 2018 wamejumuika katika viwanja vya bunge jijini Dodoma kuuaga mwili wa aliyekuwa mbunge wa Buyungu, Kigoma kwa tiketi ya Chadema, Kasugu Bilago aliyeaga dunia Jumamosi iliyopita katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu.
Akizungumza kwa niaba ya Chadema, Mwenyekiti wa Chama hicho na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freema Mbowe amewaasa wabunge na kusema kifo ni upatanisho.
“Leo tumejumuika kumuaga mwenzetu, Bilago alikuwa mbunge, kiongozi wetu lakini pia alikuwa Mwenyekiti wa Chama kwa Kanda ya Magharibi yenye mikoa mitano. Chama kimepoteza mbunge, mwenyekiti wa chama na mjumbe wa kamati kuu ya chama.
“Kifo ni fursa ya kurejesha upatanisho, tuyatafakari maisha yetu, vyote tulivyo navyo, mwisho wake ni kifo. Katika maisha yetu tunapoona mmoja wetu ametangulia mbele ya haki, sote tunakuwa wapweke,tukumbuke kuwa sote ni binadamu, na siku moja tutarudi tulikotoka,” alisema Mbowe.

No comments