CHADEMA yavuna wanachama wapya Arusha
Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Kata ya Themi Jiji la Arusha kimepokea wanachama wapya.
Akizungumza baada ya kuwakabidhi kadi wanachama hao wapya Mwenyekiti wa operesheni ya 'Chadema ni Msingi' Wilaya ya Arusha Elisante Akyoo amesema kitendo hicho kina maana kuwa chama hicho bado kinaungwa mkono na wananchi.
Akyoo amesema Chama hicho ni mbadala wa Chama kinachoongoza hivyo akawataka wananchi kuendelea kukiamini chama hicho.

- Naye Katibu Mwenezi wa CHADEMA Kata ya Themi Saidi Khatibu (Maji ya Tanga) amesema Sera ya mabadiliko inazidi kukubalika. Saidi Amesema tafsiri ya miaka mitano ya CHADEMA na miaka 50 ya CCM imeonekana Arusha kwani Mambo makubwa na mabadiliko yameonekana.
No comments