TANGAZA NASISI

Breaking News

Kivulini Maternity Center,mwarobaini wa Mama na mtoto Arusha.

Naibu waziri wa Afya,maeendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Dr Faustine Ndugulile amesema Serikali itashirikiana na Sekta binafsi zinazohusika na afya ili kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma ya matibabu kwa uboara wa hali juu.
Naibu ameyasema hayo Mapema leo Juni 9 mwaka huu wakati akizindua hospitali ya Mama na mtoto ya Kivulini Martenity Centre iliyopo kata ya Matevesi mkoani Arusha,yenye lengo la kutoa huduma za Mama na mtoto.
katika uzinduzi huo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwamo Mh Joshua Nassary mbunge wa Arumeru mashariki,Mh Godbless Lema mbunge wa Arusha Mjini ambaye ndiye mwanzilishi wa wazo la kujengwa kwa Hospitali hiyo amesema amepita milima na mabonde hadi kutimiza ndoto aliyoianza mwaka 2010 katika ujenzi wa hospitali hiyo,lengo kuu likiwa nikuokoa afya ya mama mjamzito na mtoto. Dk,Andrew Browning ambaye ni muasisi wa taasisi ya Martenity Africa alitoa wito kwa akinamama wajawazito kujifungulia hospitalini badala ya majumbani huku akisema wafadhili watajitahidi kushirikiana na serikali kuhakikisha wanafikia malengo waliyojiwekea. Naye Mwenyekiti wa Mfuko wa maendeleo ya jimbo la Arusha mjini (ARDF)Elifuraha Mtowe anashukuru kuona ndoto yao ya muda mrefu ya kujenga hospital ya mama na mtoto ikitimia,na kwa sasa wanaelekeza nguvu katika ujenzi wa shule ambayo itasaidia watoto wenye vipaji maalumu vya Michezo.

No comments