Kiwanda cha Mount Meru Millers Yapigwa faini sakata la Uchafuzi wa Mazingira , Kinabo atia Neno
Wakizungumza na Idea Radio wananchi hao wamesema suala hilo limekuwa sugu kwenye eneo hilo na kwamba wanapata adha ya kukumbana na harufu Kali ambayo hutokana na muozo wa Maji hayo machafu ambayo yanadaiwa kufunguliwa nyakati za usiku .
Eneo la barabara ambayo Maji hayo machafu yanatiririkia... |
Aidha Diwani wa Kata ya Themi Jiji la Arusha Mh. Melance Kinabo amesema wameipa Kiwanda hicho Onyo kwa kuziba matundu yote inayopitisha maji hayo kuelekea barabarani na kuhakisha Maji yote machafu kutoka kiwandani hapo hayatoki nje badala Yake watafute mbadala.
Zoezi la Uchimbaji wa mitaro maalum ya Kutiririsha Maji kwenda kwenye chemba zikiwa zinaandaliwa... |
Diwani Kinabo amesema "Tunahitaji viwanda lakini pia afya na maisha ya wananchi wetu ndo jambo la kwanza hivyo tumieiomba Kiwanda hichi kutekeleza maazimio hayo.." Alisema Mh. Kinabo
Naye katika Taarifa Yake Afisa Afya Kata ya Themi Akaeleza Historia ya tatizo tangu lilipoanza kulalamikiwa ambapo Taarifa hiyo imedai kuwa Kiwanda hicho kilishapigwa faini ya shilingi za Tanzania laki mbili (200,000) kama adhabu Fedha ambazo wameshalipia.
Jitihada zetu za kuwapata uongozi wa Kiwanda hicho ziligonga mwamba ili kuzungumzia tuhuma hizo huku jitihada zaidi zikiwa zinaendelea.
No comments