TANGAZA NASISI

Breaking News

Mungure akata Kiu ya wananchi Adha ya Ofisi ya Kijiji, Miradi lukuki ya Maendeleo nakumuunga mkono Rais JPM kwa kupiga kazi '...ataondoka MBOWE ...nitashika nafasi ya MBOWE..."


Diwani wa Kata ya Kikatiti kwenye Halmashauri ya Meru DC Mh. Elisa Mungure Amewataka watendaji wa Umma kwenye Kata Yake kutojihusisha na masuala ya rushwa katika kutekeleza majukumu ya na kutojihusisha na vyama vya  sias ili kuongeza ufanisi katika Huduma ya umma.

Akizungumza kwenye mkutano wa  kijiji cha Kikatiti ambayo uliwakutanisha mamia  ya wakazi  nakujadili masualabalimbali ya maendeleo. Suala la Afya, Elimu, na  Mazingira yalizungumzwa.

Aidha  Mungure amesema vitendo vya  rushwa kwenye Kata ya Kikatiti havijawahi kutokea na kwamba jitihada zinahitajika ili kuepukana na janga hilo  la rushwa pamoja na watendaji kutojihusisha na itikadi za vyama vya  kisiasa ili kutoa  huduma  bora kwa Jamii ya Watu wa Kikatiti.

Katika Hatua  nyingine Mungure alizungumzia sakata la watendaji wa umma ambao huenda wakawa mizigo katika Kata hiyo kwakutofanya kazi zao kwa ueledi kwa kutaka  kuhusisha vyama vya  kisiasa masuala ambayo amedai yanapelekea kukwamisha Huduma ya Jamii.

Vipaumbele vingine elekezi kwenye Mkutano huo ulikuwa pia Pamoja na ujenzi wa Ofisi za Kijiji cha Kikatiti ambapo Wananchi kwenye Suala hili walikoshwa na Diwani wao baada ya kutoa  mapendekezo ya ujenzi wa Ofisi za kijiji na kupiga marufuku ya wananchi wake kutofanyiwa tozo ya michango nakuahidi kujenga Ofisi hiyo kwa gharama zake binafsi kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo.

Licha ya Furaha kubwa ya wakazi waliohudhuria Mkutano huo Mkubwa wa kihistoria Mungure ambaye  pia ni Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Arusha Akapigilia msumari suala la kutojiuzulu kwa madai ya kumuunga Mkono Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Dr. John Pombe Magufuli nakusema ataendelea kumuunga mkono Kiongozi huyo wa Taifa kwa kufanya kazi za Maendeleo.

Hata hivyo Mungure pia Akaweka bayana kuwa hayupo tayari kukihama chama chake kwa sababu zozote zile 'Atahama MBOWE nitabaki CHADEMA.... Nina ndoto ya kushika nafasi ya MBOWE Taifa...." NUKUU

Katika kikao hicho pia Mungure aliweka bayana Miradi mbali mbali ikiwa  pamoja na ujenzi wa Vyoo katika shule za Msingi Surumala na Shule ya Msingi Chem Chem ujenzi unaigharimu kiasi cha Tsh. 30,000,000 Thelathini Millioni.

No comments