TANGAZA NASISI

Breaking News

RC Gambo azindua Zoezi la utiaji Saini Mkataba wa zaidi ya Billioni 22 Arusha Meya , Mkurugenzi wa watilia Saini

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. Mrisho Mashaka Gambo akizindua zoezi la utiwaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Barabara  kadhaa za Jiji la Arusha kama ilivyoainishwa kwenye habari hapa chini , Mradi wa zaidi ya Billioni  22.  Mkataba uliosainiwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Mh. Kalisti Lazaro na Mkurugenzi wa Jiji hilo Mh. Athumani Kihamia. Picha na Dijacson John

Kampuni ya  Sinohydro Corporation Ltd ya Nchini China  pamoja na Jiji la Arusha wamesaini mkataba wa ujenzi wa barabara ya kilomita 12.5 unaogharimu kiasi cha sh,bilioni 22.296.

Akishuhudia Zoezi la Utiliwaji wa mkataba wa makubaliano ya ujenzi huo kwa udhamini wa Benki ya Dunia (WB),Rc Gambo amewataka wataalam wa halmshauri ya Jiji wakishirikiana na viongozi kwa ujumla kutoa vipaumbele kwa barabara zenye uwekezaji mkubwaunaopatia Taifa pato kubwa na ajira kwa wananchi.
Mbunge wa Arusha Mjini Mh. Godbless Lema Kwenye hafla ya Utiaji Saini . Picha na Dijacson John.
Gambo amemwagiza Mkurugenzi wa Jiji la Arusha ,Athumani Kihamia kuhakikisha wanafanya upembuziyakinifu kwaajili ya ujenzi wa  barabara za viwandanina pembezoni ili zijengwe kwa kiwango cha  lami.
"Fanyeni vikao ili kuhakikisha mnafanya tathimini ya barabara zote za viwandani kwaajili ya uwekaji wa lami pia na nyie wakandarasi hakikisheni mnafanya kazi ya kutengeneza barabara kwa miezi 15 kama mkataba unavyoelekeza"

Alisisitiza kuwa hatarajii kuwepo kwa visingizio vyovyote baliwashirikiane na idara husika ili kujua misimu ya mvua .
Diwani wa Kata ya Themi Mh. Melance Kinabo akishuhudia zoezi la Utiaji Saini . Picha na Dijacson John.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Arusha,Gabriel Daqqaro alipendekeza barabara inayopita eneo la kuanzia Ngulelo kupitia Moshono kwenye Hospitali ya Wilaya kwenda Njiro iunganishwe kwa lami ili kuondoa msongamano kwa wananchi wanaotumia barabara hizo.

Naye Mbunge wa Arusha Mjini,Godbless Lema ameishukuru serikali kwa ujenzi wa barabara hiyo ya Ngarenaro hadi Dampo ambayo pia itapitia Veta kwenye makazi yake.

Naye Mshauri wa Mradi huo,Mhandisi Uugust Mbuya alisema ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 12.5 umegawanyika kwenye maeneo nane ikiwemo uboreshwaji wa dampo la kisasa la Muriet pamoja na uwanja wa kisasa wa michezo katika shule ya msingi Ngarenaro.
Diwani wa Kata ya Themi Mh. Melance Kinabo akionesha Mkataba uliosainiwa Na Mkuu wa Mkoa, Meya na Mkurugenzi wa Jiji la Arusha kama ishara ya kuwa umekamilika.. Picha na Dijacson John

No comments