Watoto wawili wamefariki dunia wakiogelea
Woto wawili wa kike wakazi wa Moshono katika jiji la Arusha ,wamekufa Maji wakati wakiogelea kwenyedimbwi la Mto Mokemo uliopo katika kata ya Moshono
Tukio hilo limetokea jana Majira ya saa 6 mchanawakati watoto hao walipoenda katika mto huo kwalengo la kuogelea ndipo walipoteleza na kuzamandani ya Maji.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha aliwatajamarehemu kuwa ni Deborah Ngowi (8)na AnjelaNgowi(6)wote wakazi wa Moshono
"Tulipata taarifa kutoka kwa RAIA wema kwambawatoto hao walikuwa wamezama kwenye Maji ,askari wetu walifika na kuwaokoa wakiwa hai''AmesemaKamanda
Ameongeza kuwa wakati askari wakijaribu kuwakimbiza katika hospital ya Mkoa Mount Meru kwa lengo la kuokoa maisha yao, walifariki dunia
Miili ya watoto hao imehifadhiwa katika chumba cha maiti katika hospital ya Mkoa wa Arusha ,Mount Meru
No comments