Halmashauri ya Mlele waanza kugawa miche ya Korosho kwa wakulima
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi Alexius Kagunze amesema kuwa katika jitihada za kuhakikisha wanaleta maendeleo katika Kilimo,tayari wameanza kuotosha miche ya Korosho na kuwagawia wakulima ili kupunguza kutegemea zao la tumbaku kama zao pekee la kibiashara.
Mkurugenzi Kagunze ameyasema hayo wakati alipokuwa akifanya mahojiano na GAZETI hili juu ya mikakati iliyowekwa na Halmashauri katika kuboresha sekta ya Kilimo .
Aidha amesema kuwa katika jitihada hizo Halmashauri tayari imeanzisha Kiwanda kidogo cha kuchakata Alizeti na kununua mashine ya kukamua Alizeti inayogharimu milioni kumi na tano pamoja na jengo mzuri lengo nikiwa ni kuwafanya wakulima kuwa na uzoefu wa mazao hayo na kujifunza mbinu mbalimbali za Kilimo.
Kuwa Tumbaku limekuwa ni zao kubwa katika Wilaya ya Mlele na limeonekana Kukosa soko kwani watu wanalima sana lakini katika kulipwa hela inachelewa jambo ambalo linapelekea wakulima kukata tamaa.
Kagunze amesema kuwa Halmashauri yake ambayo ni mpya inakuwa kwa kasi kutokana na utendaji makini wa watumishi wa Serikali wa awamu hii ya tano wameona vi vyema waanzishe Kilimo cha Korosho ambacho kimekuwa na soko kubwa katika nyanda za kusini mtwara na Lindi.
Kuwa mbali na jitihada za kutoa elimu kwa wakulima kupitia maafsa Kilimo wa Halmashauri wameweza kuanzisha mashamba ya Alizeti kama Kilimo cha biashara ambapo wanaendelea kuelimisha jamii kulima mazao hayo yakiwemo mahindi,Karanga pamoja na maharage ili waweze kuwa na chakula cha kutosha .
Pia ameongeza kuwa katika kuhakikisha wanafanikiwa zoezi hilo baadhi ya viongozi wa Halmashauri akiwaongoza wameweza kulima heka tano za mazao hayo ikiwa ni kuonyesha mfano kwa wananchi ili nao waweze kuwaiga viongozi hao.
Amewataka wakulima kuacha uzembe wafanye kazi kwa bidii huku wakitumia mbinu bora ambazo wanapewa na wataalamu sambamba na kulima chakula cha muda mfupi kama mihogo,mpunga jambo ambalo litasaidia kuondoka na njaa.
Kwa upande wake mmoja wa wakulima katika kijiji cha Inyonga kata ya Inyonga kilichopo ndani ya Halmashauri hiyo Julieth William amesema kuwa wanaishukuru Serikali ya Awamu hii kwa jinsi inavyowasaidia wananchi wake katika masuala ya maendeleo hasa kuwakomboa wananchi wa hali ya chini.
Amesema kuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakilima Tumbaku kama zao la biashara lakini juhudi zao zimekuwa zikigonga mwamba baada ya kucheleweshewa pesa zao na pia kutoona dhamani ya zao hilo hivyo na kudai kwamba zao la Korosho litakuwa na tija kuinua kipato chao .
Ametoa wito kwa Serikali kuwa patia pembejeo za Kilimo ambazo zimekuwa ni changamoto kubwa katika kufanikisha Kilimo chao kwani wapo wadudu waharibifu wa mazao.
MWISHo

No comments