Hotuba ya Rais Zuma yaahirishwa
Afrika Kusini imeahirisha hotuba ya rais kuhusu hali ya taifa, ambayo ni tukio muhimu la kisiasa la mwaka, wakati ambapo chama tawala cha African National Congress ANC kikizongwa na mapambano ya kumvua madaraka rais Jacob Zuma. Zuma ambaye amekuwa madarakani tangu 2009 anapigania nafasi yake na anakabiliwa na hatari ya kuondolewa karibuni na chama chake kufuatia kashfa kadhaa za rushwa.
Chama cha African National Congress kilichotawala Afrika Kusini tangu Nelson Mandela aliposhinda uchaguzi wa kwanza baada ya kumalizika kwa utawala wa ubaguzi wa rangi mwaka 1994, kimegawanyika juu ya kuondolewa kwa Zuma katika nafasi yake. Lakini kamati kuu ya chama, ambayo ndiyo chombo cha juu cha maamuzi, itakuwa na kikao maalumu kesho Jumatano kujadili uwezekano wa kumuondoa.

No comments