Mwalimu afikishwa mahakamani kwa kosa la ubakaji
MWALIMU wa shule ya ya msingi ya St Thomas iliyopo Moshono jijini hapa, David Nchemba, (25), amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Arusha kwa makosa mawili ya kumbaka na kumlawiti mwanafunzi wa kike mwenye umri wa miaka 8 anayesoma shuleni hapo.
Wakili wa Serikali, Rose Sule, aliieleza mahakama hiyo mbele ya hakimu Mkazi, Nestory Barro jana kuwa mshitakiwa alitenda makosa hayo kwa nyakati tofauti mwezi februari na Juni, mwaka jana.
Alidai kuwa Mwalimu huyo alikuwa akiwafuata watoto wakicheza na kuwaita mmoja mmoja kwa zamu wamfuate darasani kisha aliwafunika macho kwa kutumia tai yake na kuwaziba mdomo kwa kutumia mkono wake kisha kuwabaka na kuwalawiti.
Wakili Sule aliendelea kuieleza mahakama hiyo kuwa wazazi wa mtoto huyo walibaini tatizo kwa mtoto huyo wakati wa likizo ambapo walimuuliza ndipo akawaeleza kuwa alibakwa na mwalimu wake ambaye ndiyo mshitakiwa huyo.
Alidai mahakamani hapo kuwa baada ya hapo wazazi walichukua hatua kwa kuamua kutoa taarifa kwenye kituo cha polisi ambao baada ya kuchukua maelezo waliongozana mpaka shule ya St Thomas na kumkamata mshitakiwa kisha alipelekwa kituo cha polisi kwa mahojiano.
Mshitakiwa Nchemba anayetetewa na wakili, Steven Makwega alikana mashitaka hayo hivyo shauri hilo limeahishwa mpaka Machi 19, mwaka huu ambapo mshitakiwa Nchemba yupo nje kwa dhamana.
No comments