Baada ya Kutangaza Kuacha Muziki Q Chief Mzee wa upako ampigia Simu usiku wa manane
Mwanamuziki Q-Chillah hivi karibuni alitangaza rasmi kuacha muziki na kusema kuwa mambo mengi yamemtafuna na kumfanya ashuke sana kimuziki ikiwa ni pamoja na athari mbaya ya matumizi ya madawa ya kulevya.
Hata hivyo baada ya kuongea hivyo watu wengi waliguswa na historia na maamuzi yake na wengi wamekuwa wakimpigia simu, kati ya hao pia yupo Mzee wa upako ambae alimpigia sim u na kuongea nae ili kumsaidia.
“Nimepokea simu kutoka kwa mze wa upako, antony lusekelo usiku wa saa tisa unaweza kuona ni jinsi gani watu wameumia na hili anasema ameguswa sana na aliposikia alitaka kama kulia hivi. na pia nimepigiwa simu na maustadhi wakubwa sana.”Alisema Q-Chillah akiwa anaongea na clouds Tv.
Hata hivyo anasema kuwa amefikia maamuzi haya kwa kuamua yeye mwenyewe na hana kinyongo na mtu lakini tangu ametangaza kuacha muziki anaona kuwa watu walikuwa na mapenzi makubwa sana na yeye kuliko laivyokuwa akidhani.
No comments