TANGAZA NASISI

Breaking News

JACK PEMBA ATINGA DAR, ATAMBA KIBABE, AMFAGILIA JPM – VIDEO


MFANTABIASHARA maarufu Afrika Mashariki, Jack Pemba ametua jijini Dar es Saalaa na kutamba kibabe akisema Tanzania ni nyumbani alipozaliwa na kukulia hivyo anapapenda, anapaheshimu na ndiyo nchi iliyomfungulia milango ya mafanikio yake.

Katika video ambayo Global TV imeinasa, Jack Pemba ambaye amekuwa akisifika zaidi kwa kutoa misaada, kumwaga fedha kwenye sherehe mbalimbali, umiliki wake wa magari ya kifahari na nyumba za kifahari, amewasifia Marais wa Afrika Mashariki akiwemo Rais John Magufuli, Paul Kagame na Yowery Museveni kwa kazi nzuri wanayofanya ya kuongoza mataifa yao kwa amani na utulivu.

Jack Pemba ambaye pia aliwahi kuwa mpenzi wa msanii wa Bongo, Isabella Mpanda, aliingia kwenye headlines baada ya kufunguliwa kesi na tajiri mwenzake, Godfrey Kirumira wa nchini Uganda, Pedeshee Jack Marshal Pemba, jambo lililompelelkea kuyasusa magari yake matatu ya kifahari yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1.2 za Uganda.

No comments