TANGAZA NASISI

Breaking News

Sababu za Rais Mahmoud Abbas Kulazwa Hizi hapa


Leo May 21, 2018 Rais wa Palestina Mahmoud Abbas amelazwa katika hospitali moja kwenye Ukingo wa Magharibi kutokana na matatizo yaliyotokea baada ya upasuaji mdogo wa sikio aliofanyiwa wiki iliyopita.
Hii ni mara ya tatu, Abbas analazwa katika kipindi cha wiki moja.
Abbas aliwasili hospitalini baada ya kiwango chake cha joto mwilini kuenda juu.
Hata hivyo, shirika la habari la WAFA limesema kwamba uchunguzi wa kimatibabu aliofanyiwa rais huyo umeonesha kwamba hali yake ni nzuri.

No comments