Spika wa bunge Mh. Job Ndugai Ashauri wanavyuo kugombea nafasi za ubunge na udiwani
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amewashauri wahitimu wa vyuo vikuu waliokosa ajira, kugombea nafasi za udiwani na ubunge.
Spika Ndugai ametoa ushauri huo leo jijini Dodoma katika kipindi cha maswali na majibu, ambapo amesema kazi hizo za kuwawakilisha wananchi hazihitaji uzoefu.
“Kuna ajira nyingine hazihitaji uzoefu, kuna udiwani, ubunge. Najua nawatangazia vita watu wengine,” amesema Spika Ndugai.
Ushauri huo umekuja baada ya Mbunge Viti Maalumu, Zainab Katimba kulalamika kwamba vijana wengi wanakosa nafasi za ajira kutokana na masharti ya nafasi za ajira zinazotelewa kuwabana hasa kigezo cha uzoefu kazini.
Akijibu malalamiko hayo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama amesema serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo waajiri, imejipanga kuhakikisha ajira zinatolewa bila ya vikwazo ili wahitimu waweze kupata ajira.
Aidha, amesema serikali imetengeneza muongozo kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Ufundi Standi wa kutambua mahitaji ya soko la ajira ili kuwandaa vyema vijana wanaohitimu vyuo vikuu kukidhi matakwa ya soko la ajira, huku akiwataka vijana hao kutokimbilia ajira zenye vigezo ambavyo hawavimudu.
No comments