TANGAZA NASISI

Breaking News

MUNGURE AZINDUA MTAMBO WA KUSAFISHA MAJI YENYE MADINI YA FLORIDE, ASEMA ANATEKELEZA ILANI YA CHADEMA

Mtambo wa Kusafisha Maji yenye  Fluoride.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Surumala wakiwa pamoja na viongozi  mbali mbali akiwemo Diwani wa Kata hiyo na Katibu wa Chadema Mkoa wa Arusha Mh Elisa Mungure wakati akizindua mradi wa mtambo wa kusafisha Maji yenye  Fluoride (kama unavyoonekana kwenye picha) Picha na Dijacson John
Diwani wa Kata ya Kikatiti Halmashauri ya Wilaya ya Arumeru Mh Elisa Mungure Leo agosti 09 amezindua mradi wa kisima cha Maji na Mtambo  wa kusafisha Maji yenye uwingi wa madini ya Fluoride katika shule ya Msingi Surumala.
Diwani wa Kata ya Kikatiti na Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Arusha Mh Elisa Mungure (Katikati). Picha na Dijacson John.

Mungure ambaye  pia Ni Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Arusha amesema katika Kata hiyo amekuwa  akitekeleza ilani za Chama hicho ambayo hueleza kwa mapana  Masuala ya Maendeleo ya wananchi.  
Katika shule ya Msingi Surumala Mungure kwa kushirikiana na Wadau wa Maendeleo wamezindua mtambo wa kusafisha Maji yenye  fluoride ili kusaidia Kupunguza hatari  ya wanafunzi na Jamii  kuathirika na Madini ya fluoride katika Kata hiyo.

Awali  akizungumza na waandishi wa habari Mungure alifafanua kuhusu hatari  ya Madini hayo katika afya ya binadamu ambayo huathiri mifumo ya akili na Mifupa asa  kwa watoto hivyo kupatikana Kwa mradi huenda ukawa mwarobaini wa athari za fluoride kwa Jamii ya watu wa Meru.
Wananchi wa kijiji cha Surumala wakishuhudia Uzinduzi wa Mradi wa kusafisha Maji yenye fluoride. Picha na Dijacson John.

Aidha  Mwalinu Mkuu wa Shule ya Msingi Surumala Bw. Elinihaki Boni akaeleza Umuhimu wa mtambo huo wa kusafisha Maji yenye  fluoride katika shule hiyo. 

Mwalinu Elinihaki amesema Mtambo huo ni neema kubwa kwa wanafunzi wa shule hiyo ikiwa nia pamoja na kizazi kijacho.

No comments