TANGAZA NASISI

Breaking News

MUNGURE: Wanaojiuzulu kwa kigezo cha kumuunga mkono Rais 'Wanamhadaha' Rais wetu

Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA na Diwani wa Kata ya Kikatiti Mh. Elisa Mungure alipokabidhiwa zawadi ya T-shirt kutoka Chuo  cha Seoul National University kutoka Korea Kusini.
Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mkoa wa Arusha Mh. Elisa Mungure Amewataka viongozi  wanaotokana na Chama hicho kutojiuzulu nafasi zao kwa kuunga mkono juhudu  za Rais badala yake wamuunge mkono Rais kwa kufanya kazi katika nafasi walizopewa na wananchi na kwamba kitendo cha kumuunga mkono Rais kwa kujiuzulu ni kumkejeli na kumhadaha Rais.

Mungure ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kikatiti amesema hayo akizindua mradi wa kisima cha Maji na mtambo  wa kusafisha maji yenye  madini ya Fluoride katika shule Msingi Surumala na mradi wa  umeme wa jua Kwenye shule  Sekondari Kikatiti miradi ambayo imefanikiwa kwa jitihada za Diwani ,na  chuo  kikuu cha Masuala ya kijamii mjini Seoul Nchini Korea Kusini.
Wanafunzi wa Chuo  cha Seoul national University kwenye Maagano na Wananchi na wanafunzi wa shule ya Sekondari Kikatiti.

Naye Mwalinu Mkuu wa Shule Sekondari Kikatiti Tareto Nasari licha ya wa kumshukuru Diwani na wafadhili hao  Amesema mradi huo wa umeme wa jua utawasaidia katika kuhakikisha wanafunzi wanapata muda mzuri  wa kusoma hata nyakati ambazo kuna changamoto ya umeme shuleni hapo.

No comments